Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeshtakiwa kumwibia mbunge aachiwa huru

Wee Jail Aliyeshtakiwa kumwibia mbunge aachiwa huru

Sat, 20 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Mwanzo Maromboso jijini hapa, imemwachia huru mfanyakazi wa ndani, William Mlewa, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya wizi wa shilingi milioni saba za mwajiri wake, Anjela Kizigha, mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki baada ya kumkuta hana hatia.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu wa Mahakama hiyo, Neema Mchomvu, alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umeshindwa kujitosheleza kuishawishi mahakama hiyo kumtia hatiani mshtakiwa.

Alisema mashahidi sita wa upande wa mashtaka wameshindwa kuthibitisha mashtaka, hivyo mahakama imeona mshtakiwa hana hatia na kumwachia huru.

Awali, mlalamikaji wa shauri hilo, Kizigha, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa, alikuwa mfanyakazi wake wa ndani kwa nyakati tofauti na alimwibia kiasi hicho cha fedha na baada ya tukio hilo, alijizuru kwa kujitumbukiza kwenye sufuria la uji wa moto kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Hakimu Mchomvu alidai kuwa upande wa mashtaka unaweza kukata rufani ndani ya siku 30 kama haujaridhika na uamuzi wa mahakama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live