Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyesababisha vifo vya walevi afikishwa kortini

Vifo Vya Walevi higela Ngelanija

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Lindi, imemsomea shtaka moja la mauaji mganga wa kienyeji aitwaye Shigela Ngelanija, anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji ya watu watano ambao walimfuata awape dawa ya kunywa ili waache pombe, na baadaye kufariki dunia baada ya kunywa dawa hiyo.

Shtaka hilo amesomewa hii jana Februari 2, 2023, na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Consolata Singano ambapo mtuhumiwa hakutakiwa kutaja chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Kesi ya Shigela itatajwa tena Februari 15, 2023. Vifo vya watu hao vilitokea Januari 29, 2023, katika Kijiji cha Nambilanje wilaya ya Ruangwa. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live