Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeoa mwanafunzi apandishwa mahakamani

15314 PIC+KUOA TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mkazi wa kijiji cha Iseresere wilayani Serengeti mkoani Mara, Peter Marko (30) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Serengeti mkoani humo kwa kosa la kuoa mwanafunzi wa shule ya sekondari.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyo, Ismael Ngaile mwendesha mashitaka wa Polisi, Renatus Zakeo amesema Marko alitenda kosa hilo Mei, 2018.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 231/2018, inadaiwa mshitakiwa alimuoa mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari Kisaka kinyume cha sheria.

Mshitakiwa amekana kosa na amepelekwa mahabusu, kesi hiyo ambayo upelelezi haujakamilika imeahirishwa hadi Septemba 17, 2018.

Chanzo: mwananchi.co.tz