Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemwingilia mgonjwa wa akili jela miaka 15

Afungwa Miezi 15 Jela Kwa Kusumbua Majirani Kwa Sauti Ya Juu Ya Muziki.png Aliyemwingilia mgonjwa wa akili jela miaka 15

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Mkoa wa Vuga, imemhukumu mshtakiwa ambaye ni mkazi wa Hawai Zanzibar, Said Salum (28), kutumikia kifungo cha miaka 15 Chuo cha Mafunzo na kulipa fidia ya shilingi Milioni Moja kwa kosa la Kumuingilia kimwili mgonjwa wa akili.

Akisoma maelezo ya hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama, Nayla Abdulbasit Omeyar amesema amejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba, ambao haukuwa na shaka uliomtia mshtakiwa hatiani.

Said alishtakiwa kwa kosa la kumuingilia kimwili mgonjwa wa akili kinyume na kifungu namba 133 cha sheria ya adhabu 6/2004 na kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani tarehe Julai 1, 2019 na kupewa kesi namba 203/2019.

Awali ilidaiwa kuwa, Desemba 2, 2017 majira ya saa 11:00 Jioni huko Hawai Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, mshtakiwa alimuingilia mwanamke mwenye ugonjwa wa akili, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live