Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua ndugu yake bila kukusudia ahukumiwa miaka mitatu jela

95500 Pic+kuua Aliyemuua ndugu yake bila kukusudia ahukumiwa miaka mitatu jela

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga imemhukumu mkazi wa Kijiji cha

Lunguza wilayani Lushoto, Jafari  Kijangwa (45) kwenda jela miaka

mitatu baada ya kukiri shitaka la kumuua ndugu yake Ibrahim Kijangwa

bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa leo Jumatano Februari 12, 2020 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amir Mruma  kufuatia kuanza kwa shughuli za mahakama kwa mwaka wa sheria wa 2020.

Jaji Mruma amesema Jafari itabidi aende jela miaka mitatu ambapo licha kwamba hakukusudia lakini alifanya uzembe uliosababisha kifo cha ndugu yake.

Pia Soma

Advertisement

“Hasira hasara na kama Jafar  asingechukua hatua ya kumpiga ndugu yake kusingetokea kifo na katika hili jamii inapaswa kujifunza kwamba siyo kila jambo linatakiwa kutatuliwa kwa kipigo,” amesema Jaji Mruma.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebeca Msalangi

kuwa Mei 26 mwaka 2019 katika kijiji cha Lunguza kilichopo Wilaya ya

Lushoto mkoani Tanga mshtakiwa huyo alimshambulia Ibrahim baada ya kumwaga ndoo ya mafuta ya kukaangia chipsi.

Aliendelea kudai baada ya kumwaga mafuta hayo ukaanza ugomvi uliopelekea wawili hao kupigana na hatimaye Ibrahim alikufa.

Chanzo: mwananchi.co.tz