Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mwanae, kumchemsha vipande apandishwa mahakamani

64244 PIC+KIZIMBANI

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Happiness Shedrack (36) mkazi wa kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita anayetuhumiwa kumuua mwanae kwa kumkatakata vipandevipande kisha kumchemsha jikoni amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka la mauaji.

Mshatakiwa huyo alifikishwa mahakamani jana Jumatatu Juni 24, 2019 na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Geita, Nimrod Kurwijila .

Mwanasheria wa Serikali Masambu Daniel alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002

Akisoma maelezo ya kosa mwanasheria wa serikali alidai mahakamani hapo kuwa mnamo Juni 21, 2019 huko Buligi wilaya na mkoa wa Geita mshatakiwa alimuua Martha Jacob.

Mshatakiwa hakupaswa kujibu lolote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza na kuamua mashauri ya mauaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz