Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mkewe na kumbebesha kesi mwanaye atupwa jela miaka 29

Amidu Koroma Da Aliyemuua mkewe na kumbebesha kesi mwanaye atupwa jela miaka 29

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Amidu Koroma (48) Mwanaume mwenye asili ya Sierra Leone aliyemuua mke wake Mariam Kamara (46)na kumsingizia mtoto wao wa kiume, amehukumiwa kifungo kisichopungua miaka 29.

Mnamo Januari mwaka jana, kwa kutumia kisu cha jikoni Koroma alimchoma mke wake mara nne usoni,shingoni na kifuani wakati Mama huyo akiwa amelala kitandani.

Baadaye mwanaume huyo alichukua mafuta ya petroli na kuwasha moto ili kuficha kile alichokitenda.

Koroma alimlaumu mtoto wao wa kiume Ishmael (19) aliyekuwa amelala ndani ya nyumba hiyo jijini London. Mwanaume huyo alidai mtoto wao ana matatizo ya akili na anakopi maigizo aliyoyaona kwenye mtandao wa Netflix.

Baada ya uchunguzi wa kina, mwanaume huyo amekutwa na hatia ya kumuua Mariam aliyekuwa Muuguzi nchini Uingereza kwa kumchoma visu na moto.

Waendesha Mashtaka walipewa taarifa kuwa mahusiano ya wawili hao hayakuwa mazuri na Bi.Mariam alikwisha lalamika mara kadhaa kwa marafiki zake juu ya hofu aliyokuwa nayo juu ya uwezo wa mume wake kumdhuru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live