Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mama yake kwa fikira za kichawi afikishwa kortini

Nicholas Aina Nicholas Aina na Bi. Caroline Adeyelu.

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume aliyemuua Mama yake kutokana na fikira za kuwa alikuwa akitumia uchawi kumdhuru amewekwa kizuizini na atakaa hospitali kwa muda usiojulikana kwani ugonjwa alionao unaweza kusababisha hatari.

Nicholas Aina (28) alimuua mama yake mzazi Bi. Caroline Adeyelu (64) na kumchoma kisu dada yake Angel Adeyelu (23) mara saba mnamo Oktoba 2022 katika jiji la London.

Taarifa zilizofikishwa Mahakamani zinaeleza kuwa Nicholas alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kuchanganyikiwa na kuwaza uchawi na masuala mengine yasiyokuwepo.

Mwanaume huyo mwenye asili ya Nigeria amekuwa na historia ya kufanya vurugu kwa familia yake, aliwahi kumpiga dada yake na taa kichwani, na aliwahi kumtishia mama yake kwa kisu.

Kwa mujibu wa dada yake, Nicholas aliacha kutumia dawa za akili siku chache kabla ya tukio na hali yake ilizidi kuwa mbaya.

Akiitaja hukumu ya kesi hiyo, jaji David Aubrey alisema kuwa, "Umesababisha matatizo na mateso makubwa kwenye familia yako, lakini adhabu yako itapungua kwakuwa ulitenda mambo yale kutokana na matatizo yako ya akiliā€.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live