Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemmwagia maji ya moto mke mwenza ahukumiwa miaka mitatu jela

Hukumu Pc Data Aliyemmwagia maji ya moto mke mwenza ahukumiwa miaka mitatu jela

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu miaka mitatu jela Vumilia Kasomelo (32) kwa kosa la kumjeruhi kwa maji ya moto mke mwenza, Mariam Paul (36).

Hukumu hiyo imetolewa Septemba 5, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Evod Kisoka katika kesi ya jinai namba 109/2023 baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo Agosti 26 mwaka huu saa 3 usiku akiwa kwenye msiba wa baba mkwe wao, Costantine Sululu.

Akisoma mashtaka dhidi ya Vumilia, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Morice Mtoi amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo la kummwagia maji ya moto mke mwenzake katika kijiji cha Lugata, tarafa ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

Amesema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 toleo la mwaka 2022.

Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo akidai kutenda kutokana na hasira baada ya kuoneshwa na watu waliokuwa kwenye msiba wa baba mkwe wao kuwa Mariam ni mke mwenzie kwa mume wao, Ndagabwene Evarist (38) ambaye hata hivyo hakuwahi kumuona au kufahamishwa na mume wake.

Licha ya Vumilia kuomba kupunguziwa adhabu, Mahakama imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live