Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemkata mkewe kwa chupa usoni akamatwa

Aliyemkata mkewe kwa chupa usoni akamatwa

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Marwa Maduka, mkazi wa Rung’abure Wilaya ya Serengeti aliyetoroka baada ya kudaiwa kumkata mkewe kwa chupa kutokana na wivu wa mapenzi  amekamatwa akifanya kibarua katika mgodi wa dhahabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Februari 13, 2020 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema Maduka alikamatwa Februari 11, 2020 katika mgodi mdogo wa dhahabu ulioko kijiji cha Merenga.

Maduka alitoroka Februari 3, 2020 baada ya kumpiga kisha kumkata kwa chupa usoni mkewe, Esther Makenge (19) kwa madai wa kuchelewa kurudi nyumbani akitoka kwenye biashara zake.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Merenga, Moses Ryoba amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na baadhi ya wachimbaji mgodini hapo kumtambua, kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi Machochwe.

Akizungumza na Mwananchi akiwa hospitalini,  Esther amesema mumewe alimtuhumu kuwa alichelewa kurudi nyumbani kwa sababu alikuwa na wanaume wengine.

“Baada ya kunipiga ngumi na mateke, alichukua chupa ya bia akanipiga nayo na ilipopasuka akaanza kutumia kipande kunikata  usoni,” amesema Esther.

Pia Soma

Advertisement
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa awali wa tukio hilo kukamilika.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz