Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyembaka na kumnyonga mke wa mtu ahukumiwa kunyongwa

Pingu Law Aliyembaka na kumnyonga mke wa mtu ahukumiwa kunyongwa

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama kuu kanda ya Iringa imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Mohamed Njali, kwa kosa la kukutwa na hatia ya kubaka na kumuua kwa kumkaba shingoni Atika Chesco Kivanule, mwenye umri wa miaka 24 majira ya saa saba usiku wakati mumewe akiwa anatazama pambano la ngumi.

Njali alitenda kosa hilo Septemba 24, 2022 majira ya saa 7 usiku baada ya kuvunja mlango kisha kuiba simu na suti baadaye kumbaka na kumnyonga shingoni Bi Atika.

Baada ya kutekeleza unyama huo, akiwa anatoka alikutana na shemeji wa marehemu na alipoanza kukimbia ndipo taratibu taratibu za kwenda kituo cha polisi utoa taarifa na kwa mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa zikafanyika.

Mtuhumiwa alifanikiwa kukamatwa akiwa chumbani kwake na baada ya ukaguzi alikutwa na suti pamoja na simu ya marehemu.

Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi nane akiwemo daktari ambaye ni shahidi namba nne aliyeupokea mwili wa marehemu ambaye ameiambia mahakama hiyo kuwa, marehemu alifariki kutokana na ubongo kukosa hewa kutokana na kunyongwa shingoni.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Juma Kamakuu Angaza Mwipopo amesema kuwa kosa hilo halina adhabu mbadala kwani adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.

Akizungumza mara baada ya kutolewa hukumu hiyo, mume wa marehemu Adiline Kileo ameishukuru mahakama kwa kutoa hukumu hiyo.

“Hukumu hii nimeipokea kwa furaha na majonzi kwa sababu lengo langu ilikuwa ni kutafuta haki ya mke wangu na mtoto wangu aliyekufa na mke wangu, ambayo ilitokea mwaka jana.

“Niliumia sana, niliteseka sana, mtoto wangu wa miaka mitano ambaye alishuhudia kifo cha mama yake ameteseka sana, nimehangaika sana kumuweka sawa kiakili, ninamshukuru Mungu nimemuweka sawa na mimi pia niko sawa na roho yangu imetulia.

“Nskumbuka machungu makubwa sana siku ile siwezi kuisahau mpaka naingia kaburini, najilaumu sana kutoka siku ile na kuiacha familia yangu nyumbani,” amesema Kileo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live