Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyembaka mjamzito ahukumiwa jela miaka 30

Mjamzito Aliyembaka Aliyembaka mjamzito ahukumiwa jela miaka 30

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela Agustino Kahise Mkazi wa changalawe baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka Binti Mjamazito (18) ambaye alikuwa amelazwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Mji Mafinga.

Akisoma maelekezo yaliyotolewa Mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Sekela Kyungu amesema kuwa mnamo Aprili 13, 2023 majira ya usiku katika eneo la choo cha wodi ya wazazi katika hospital ya mji wa Mafinga bila uhalali mshitakiwa alimbaka binti huyo bila ridhaa yake.

Aidha kyungu ameeleza kuwa baada ya muhanga huyo kumaliza kujisaidia wakati anatoka chooni kwa ajili ya kwenda wodini ndipo alikutana kijana huyo kwenye mlango wa chooni na kumzuia asitoke na kumziba mdomo ili asiweze kupiga kelele kisha akambaka

Hakimu huyo amesema mshitakiwa huyo ameshitakiwa kwa kosa la ubakaji ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 kifungu kidogo cha 1 na cha 2)(e) na kifungu 131 kifungu kidogo cha (1) cha sheria za kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022.

Kwa upande Mshatakiwa aliposomewa shikta lake alikana kutenda kosa hilo ndipo Mahakama ikaalika upande wa Mashkta ili waweze kuthibitisha shitaka hilo ambapo waliwasilisha vielelezo viwili pamoja na mashaidi watano.

Baada ya ushahidi ambao umetolewa kwa pande zote mbili , Mahakama imeona upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha shitaka lake bila kuacha shaka lolote na kumtia hatiani kwa kifungu namba 235 kifungu kidogo cha (1)cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 rejeo la Mwaka 2022.

Hata hivyo hakimu Kyungu amesema kulingana na kosa ambalo amelifanya mshtakiwa Mahakama hiyo inatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 Jela chini ya kifungu 131 kifunngu kidogo cha (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la Mwaka 2022 ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na wenye tabia kama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live