Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyembaka mama yake ahukumiwa miaka 30 jela

48666 Aliyebakapic

Tue, 26 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Linaweza kuwa ni tukio la kushangaza, lakini ushahidi uliotolewa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Serengeti umethibitisha pasi na shaka kuwa Chora Samson (27), alimbaka mama yake mzazi.

Hivyo, haikuwa ajabu kwa kijana huyo wa kijiji cha Burunga, kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa hilo la nadra kutokea nchini kumbaka Rhobi Nyang’ombe, mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 65.

Kabla ya Hakimu Mkazi Ismael Ngaile kusoma hukumu hiyo, mwendesha mashtaka wa Serikali, Renatus Zakeyo aliikumbusha mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 26, 2017 saa 3:00 usiku.

Zakeyo alidai katika kesi hiyo ya jinai namba 8/2018 kuwa baada ya Chora kukamatwa alifunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani, lakini akakana kosa hilo.

Mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo alichofanya hakikubaliki katika jamii.

Alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya hakimu kusoma hukumu, Chora aliiomba mahakama imuonee huruma kwa kumpunguzia adhabu, akidai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na ana watu wanaomtegemea nyumbani kwake.

Hata hivyo, Hakimu Ngaile alisema utetezi wake hauna nguvu ya kuishawishi mahakama isitoe adhabu kali, na ndipo akamsomea hukumu hiyo itakayomuweka nyuma ya nondo za gereza kwa miaka 30.

Hakimu alisema milango ya rufaa iko wazi kwa mshtakiwa kama hakuridhika na adhabu hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz