Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa mhasibu Kasulu kizimbani

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kigoma imemfikisha mahakamani aliyekuwa mhasibu mkuu halmshauri ya wilaya ya Kasulu, George Mzuma kwa tuhuma za ubadhirifu wa Sh11.7 milioni.

Akizungumza leo Januari 25, 2019, kamanda wa Takukuru mkoani hapa Raphael Mbwambo, amesema mhasibu huyo pia anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za mradi wa Ukimwi kiasi cha Sh25 milioni za mwaka 2018.

Kamanda Mbwambo amesema mhasibu huyo amefikishwa mahakama ya wilaya ya Kasulu na kusomewa mashtaka mawili ikidaiwa kuwa fedha hizo (Sh 11.7 milioni) ni za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Amesema katika kesi hiyo namba 28 ya mwaka 2018 mhasibu huyo amefunguliwa makosa mawili moja ni la kuandaa stakabadhi ya malipo ya uongo kwamba ameweka fedha hizo katika akaunti ya maendeleo ya halmashauri hiyo.

Mbwambo amesema mhasibu huyo amerudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili waliotakiwa kusaini dhamana ya Sh 5 milioni kila mmoja.



Chanzo: mwananchi.co.tz