Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa meneja Benki ya Wanawake kusota rumande

40383 Menejapic Aliyekuwa meneja Benki ya Wanawake kusota rumande

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa meneja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) tawi la Mkwepu, Priscus Shirima (37) anayekabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha fedha, anaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika.

Shirima anakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya miamala ya uongo akiwa mtumishi wa benki hiyo, wizi na kutakatisha fedha kiasi cha Sh120 milioni.

Wakili wa Serikali, Sada Mohamed amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisitu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hilo hadi Februari 20 mwaka huu itakapokuja tena.

Katika shtaka la kwanza Shirima anadaiwa kuwa Juni 20, 2016, katika Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) tawi la Mkwepu, wilaya ya Ilala, akiwa Meneja wa tawi hilo, akiwa na nia ya uovu, alifanya muamala wa uongo kwa kuhamisha Sh120 milioni kutoka akaunti namba 0310137001 ambayo ni ya Florah Lyatuu kwenda akaunti namba 0380073121, ambayo ni yake.

Katika shtaka la pili ambalo ni wizi akiwa mtumishi wa benki hiyo, Shirima anadaiwa, Juni 20, 2016 katika benki hiyo, akiwa meneja wa tawi hilo aliyeajiriwa na benki hiyo, aliiba Sh120 milioni.

Shtaka la tatu la utakatishaji fedha, mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Juni 2016, katika benki hiyo,

Mshtakiwa alijihusisha na muamala wa Sh120 milioni kwa kuruhusu na kufanya malipo kutoka akaunti namba 0380073121 inayomilikiwa na shirika, akilipa kampuni ya Sekorizi Ltd kupitia hundi tatu zenye namba 000127, 648806 na 1648791, huku akifahamu kuwa fedha hizo si halali.

Soma Zaidi: Kesi ya meneja wa zamani Benki ya Wanawake yapigwa kalenda



Chanzo: mwananchi.co.tz