Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa bosi PSSSF akutwa na kesi ya kujibu

Hukumu Pc Data Aliyekuwa bosi PSSSF akutwa na kesi ya kujibu

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Meneja wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Rajabu Kinande na wenzake wanne.

Mbali na Kinande washtakiwa wengine ni Ashura Kapera (37), Farida Mbonaheri (34), Mohamed Miraji (48) na Msafiri Raha ambapo wanakabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuvunja duka.

Wakili wa Serikali, Michael Ng'oboko amesema leo Desemba 16 kuwa utoaji wa ushahidi katika shauri hilo umekamilika.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi, Fadhili Luvinga amesema washtakiwa hao wamekutwa na kesi ya kujibu hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea.

Luvinga amesema washtakiwa hao wataanza kujitetea kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari Mosi hadi Januari 3, 2023.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Januari Mosi, 2023 Kwa ajili ya kuanza kujitetea.

Katika kesi ya msingi kati ya Juni 16, 2020 mtaa wa Gerezani Wilaya ya Ilala, washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuvunja na kuingia kwenye duka la Mohamed Soli kwa nia ya kuiba.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwemo viyoyozi vyenye thamani ya Sh830, 000 mali ya Salehe Selemani.

Chanzo: Mwananchi