Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekutwa na meno 6 ya tembo atiwa mbaroni

MBARONI.jpeg Aliyekutwa na meno 6 ya tembo atiwa mbaroni

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Katika kukabiliana na mtandao wa wizi wa nyara za Serikali, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kukutwa na meno sita ya tembo wilayani ya Same.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 14 mkoani hapa, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea za kukabiliana na matukio ya uhalifu katika mkoa huo.

Amesema pamoja na kukamata meno hayo ya tembo, pia zimekamatwa komputa mpakato 27 za wizi zilizoibiwa katika maeneo tofauti ya mkoa huo, televisioni nne na simu za mkononi tano zilizoibiwa kwenye matukio tofauti.

"Pamoja na operesheni hiyo tumebaini mtandao wa wizi wa pikipiki na tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita, akiwemo mtuhumiwa mmoja mwanaume kwa kesi ya mauaji aliyekimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kufanya mauaji na kupora pikipiki hivi karibuni wilaya ya Rombo," amesema.

Aidha Kamanda Maigwa, amesema katika operesheni hiyo kuanzia Januari hadi Februari wamefanikiwa kukamata pikipiki 15 zidhaniwazo kuwa ni mali za wizi pamoja na gari moja aina ya Toyota Land Cruiser Prado.

"Tumekamata wengine saba wanaojihusisha kupokea na kununua pikipiki za wizi, eneo la Tarakea, Hedaru na Manoro Tanga na watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani," amesema.

Chanzo: mwanachidigital