Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekutwa na fuvu, sehemu za siri tano za binadamu afutiwa kesi

Hukumu Pc Data Aliyekutwa na fuvu, sehemu za siri tano za binadamu afutiwa kesi

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemfutia kesi na kumwachia huru mshtakiwa Salum Nkonja (23) maarufu kama Emmanuel Nkonja, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na vipande viwili vya mafuvu ya kichwa cha binadamu pamoja na sehemu za siri tano za mwanamke baada ya kesi hiyo kuahishwa kwa zaidi ya mara tano bila kuendelea na ushahidi.

Umauzi huo umetolewa leo Jumatatu, April 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 32/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na kumfutia mashtaka na kumwachia huru, mshtakiwa hiyo, Mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa asikamatwe mpaka upande wa mashtaka watakapowasilisha vielelezo mahakamani.

Chanzo: mwanachidigital