Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekamatwa kwa kuendesha gari amelewa, achapa usingizi mahakamani

Usingizi Mwee.jpeg Aliyekamatwa kwa kuendesha gari amelewa, achapa usingizi mahakamani

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sharon Oparanya; ni mrembo wa nchini Kenya ambaye Mahakama Kitengo cha Trafiki imelazimika kuahirisha kesi yake ya uhalifu baada ya kuwasili kortini akiwa amelewa chakari na kutandika usingizi wa pono.

Imemlazimu hakimu kusitisha kesi hiyo kwa muda baada ya Oparanya kusikika akikoroma kwa nguvu kortini.

Baada ya kuona hali hiyo, hakimu alitoa agizo kwa Oparanya kuwekwa rumande hadi pombe itakapokuwa imeisha mwilini ili aweze kujibu shtaka linalomkabili la kukamatwa akiendesha gari akiwa mlevi chakari.

Hakimu Martha Nanzushi aligundua kwamba Oparanya alikuwa amelewa kiasi cha kushindwa kujibu mashtaka yanayomkabili.

“Hebu subiri, subiri kidogo! Kwa nini mshukiwa anakoroma? Je, ni nani huyo anayelala mbele yangu nikiendesha kesi?” Hakimu huyo aliuliza.

Ofisa wa Polisi aliyemkamata Oparanya alithibitisha kuwa ni kweli kwamba alikuwa mlevi.

Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa mahakamani na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Oparanya anatuhumiwa kuwa mnamo Septemba 22, 2022, saa 1:35 Asubuhi kwenye Barabara ya Ngong, alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili KDH 250R aina ya Mercedes-Benz, kwa mwendo wa kasi, tena akiwa mlevi na kushindwa kulithibiti gari hilo. Alipopimwa kubaini kiwango cha pombe mwilini mwake, ilbainika kwamba ilifikiwa kiwango cha 0.978mg /L.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live