Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejipatia mkopo milioni 350 ahukumiwa kifungo cha nje

IMG 20220406 WA0108 Aliyejipatia mkopo milioni 350 ahukumiwa kifungo cha nje

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Mkurugenzi wa Mikocheni Shopping Mall Ltd, John Kyenkungu (67) kifungo cha nje cha miezi 18, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia mkopo kutoka benki ya Equit wenye thamani ya Sh350 milioni.

Pia, mahakama imeelekeza hati iliyotumika kuchukulia mkopo, irudishwe Mikocheni Shopping Mall Ltd, ambao ndio wamiliki wa hati hiyo kwa sasa.

Kyenkungu ambaye ni mfanyabiashara pia, anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo muhtasari wa kikao cha bodi, fomu ya kusajili hati ya kiwanja na kughushi dhamana ambayo inatolewa na taasisi ya fedha.

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni 30, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Evodia Kyaruzi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya hukumu.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Tumaini Maingu, umedai kuwa haujaridhishwa na adhabu iliyotolewa dhidi ya mshtakiwa huyo, hivyo wanakata rufaa kupinga adhabu hiyo.

Chanzo: Mwananchi