Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejifanya mwanamke ili kupata kazi akamatwa kwa kumlawiti mtoto wa bosi

AJIFANYA DADA D Aliyejifanya mwanamke ili kupata kazi akamatwa kwa kumlawiti mtoto wa bosi

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja aliyejifanya kuwa mwanamke ili kupata kazi ya ndani kama kijakazi amekamatwa baada ya kujaribu kumlawiti mpwa wa tajiri wake.

Mwanaume huyo aliyetambuliwa kama Christoher Mukutindwa mwenye umri wa miaka 29 alijifanya kama mwanamke kwa sauti, kujipodoa na mavazi, ndipo akapata kazi kama mjakazi wa ndani, kazi ambayo ameifanya kwa miezi mitano kabla ya kufanya kitendo hicho cha unyama kwa mpwa wa bosi wake mwenye umri wa miaka 19.

Kulingana na taarifa zilizoripotiwa nchini Zambia, Mukutindwa alimdanganya kijana huyo na kumuingiza kwenye chumba chake kabla ya kujaribu kufanya unyama huo ila kijana huyo alimpiga mweleka na kumshinda nguvu kabla ya kukimbia na kuripoti kitendo hicho kwa bosi wa Mukutindwa.

“Ukweli ni kwamba kijakazi huyo kwa majina Christopher Mukutindwa ambaye ameajiriwa kama kijakazi kwa muda wa miezi mitano sasa alimwita mwathiriwa chumbani kwake.

"Kisha akavua kitenge alichokuwa amevaa ili apate kumtendea unyama huo na ilikuwa wakati huo ambapo mwathirika aligundua kuwa mjakazi alikuwa ni yeye na alijaribu kuhangaika, na kumlawiti, lakini aliweza kumshinda," jarida hilo lilimnukuu msemaji wa polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live