Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyejaribu kunajisi mwanafunzi afungwa

Aa49588e8a81603331ae13e1c35cd45f Aliyejaribu kunajisi mwanafunzi afungwa

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemhukumu mkazi wa kijiji cha Mwazye, Chrisant Longwani (32) miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kujaribu kumnajisi mwanafunzi wa kike (11) wa darasa la nne.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Nickson Temu alisema ametoa adhabu hiyo baada ya mshitakiwa kukiri kosa lake. Alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 132 (1) cha Sheria, Kanuni ya Adhabu.

Alisema mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka ambao haukuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo.

Awali Mwendesha Mashtaka, Rajab Ndunda alidai mahakamani hapo mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka huu usiku ambapo alimvamia msichana na kurarua nguo zake.

Akijitetea mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa la kwanza ana familia kubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz