Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeingia Tanzania bila kibali ahukumiwa miezi mitatu jela

Hukumu Pc Data Aliyeingia Tanzania bila kibali ahukumiwa miezi mitatu jela

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Guinea, Lamine Nabe (34) amehukumiwa kulipa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kuishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali.

Mbali na kupewa adhabu hiyo, Mahakama pia imeamuru mshtakiwa huyo baada ya kutumikia adhabu hiyo, arejeshwe nchini kwao.

Nabe amehukumiwa kifungo hicho leo, Oktoba 21, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukiri mashtaka yake na mahakama kumtia hatiani.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira, baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani mshtakiwa kama alivyoshtakiwa.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea kwanini Mahakama hiyo isimpe adhabu kali.

Mshtakiwa Nabe hakuweza kujitetea na badala yake alidai ni kweli alikamatwa nchini na hana hati ya kusafiria wala nyaraka yoyote inayomuonyesha kuwa ameruhusiwa kuishi nchini.

Kutokana na utetezi wake, hakimu Rugemalira alimtia hatiani na kumuona mshtakiwa huyo kuwa ni mkosaji na kumpa adhabu ya kwenda jela miezi mitatu au alipe faini ya Sh 1milioni

" Mahakama imekutia hatiani katika makosa yote mawili, hivyo shtaka la kwanza ambalo ni kuingia nchini bila kuwa na hati ya kusafiria, Mahakama imekuhukumu kulipa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi mitatu na shtaka la pili ambalo ni kuishi nchini bila kuwa na kibali, unahukumiwa kulipa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi mitatu na kwamba adhabu hii inakwenda kwa pamoja hivyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda jela miezi mitatu," amesema hakimu Rugemalira.

Awali, wakili kutoka Idara ya Uhamiaji, Hadija Masoud aliiomba mahakama itoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo.

Akimsomea hati ya mashtaka, Wakili Masoud, amedai kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa Oktoba 3, 2022 eneo la Ubungo katika ofisi za Uhamiaji za wilaya hiyo.

Anadaiwa katika shtaka la kwanza siku na eneo hili, mshtakiwa akiwa raia wa Guinea mshtakiwa anadaiwa kuingia na kuishi nchini bila kuwa na kibali au nyaraka yoyote inayoonyesha uhalali wa yeye kuishi nchini.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake alikiri na ndipo aliposome hoja za awali (PH).

Baada ya kukiri mashtaka na kutiwa hatiani, Mahakama ilimtia hatiani na kisha kumhukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live