Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyehukumiwa miaka 30 jela aachiwa huru

Mizani Ya Haki Aliyehukumiwa miaka 30 jela aachiwa huru

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru Miraji Omary, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15

Awali Mahakama ya Wilaya ya Temeke ili mhukumu mshitakiwa huyo kwenda miaka 30 jela baada ya kutiwa hatia.

Mshitakiwa huyo alikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga adhabu hiyo iliyotolewa katika mahakama hiyo akidai hakimu aliyemtia hatiani alikosea.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, amesema kuwa anakubalina na rufaa hiyo, kwa sababu upande wa Jamuhuri umeshidwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshitakiwa huyo, pamoja na ushahidi kutojitosheleza.

"Ushahidi uliotolewa na mtoto huyo una mapungufu, na hauonyeshi kiundani ni namna gani alikuwa akifanyiwa kitendo hicho," amesema Msumi.

Aidha amesema mhanga huyo alidai alikuwa anabakwa kwenye nyumba ambayo haijaisha lakini shahidi ambaye ni askari polisi mpelelezi aliieleza mahakama kuwa alipotembelea nyumba hiyo, alikuta imekamilika.

"Hivyo kuna ukinzani kwenye ushahidi huo, hauelezi nyumba hiyo iko wapi na haulezi ni wakati gani alikuwa akipelekwa katika nyumba hiyo," amesema Msumi.

Msumi amesema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa shahidi namba moja, hakueleza nyumba hiyo iko maeneo gani na kuna majirani gani, na kwamba iko mbali kiasi gani kutoka saluni alipokuwa akitoka mrufani hadi katika nyumba hiyo.

Amesema shahidi huyo hakuwa na maelezo mengine mbali na kusema amebakwa na mtu huyo na hakuna uhusiano wote unaothibitisha kwamba alibakwa zaidi ya maneno ya mdomoni.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, mahakama hiyo imeona upande wa mashtaka haujaweza kuthibitisha kosa kutendeka, na kwamba ushahidi pia umeshindwa kuthibitisha mashtaka yanayomkabili.

Hivyo, Hakimu Msumi amesema anakubaliana na rufaa hiyo ambapo mrufani aliiomba mahakama hiyo imuondolee adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na pia aondolewe jela isipokuwa kama ana kosa lingine.

Kesi ya msingi inadaiwa Agosti 7, 2020 maeneo ya Temeke akiwa katika nyumba ambayo hajakamilika alimbaka mtoto wa miaka 15

Chanzo: Mwananchi