Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyehukumiwa maisha jela aruhusiwa kwenda kumpa mimba mkewe kisha arudi gerezani

Jela Maisha India.jpeg Gerezani

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jamaa anayetumikia kifungo cha maisha jela mahakama yampa ruhusa siku 15 kurudi uraiani kumpa mimba mke wake kisha arudi jela.

Mwanaume husika kwa jina la Nandlal (34) , mke wake kwa jina la Rekha ameenda kuililia mahakama ya Jodhpur/Rajasthan nchini India akitaka apewe mimba na mume wake anayetumikia kifungo cha maisha jela.

Mahakama iliamua kupitia vifungu kadhaa vya sheria na imani mbalimbali za kidini ikiwemo Uhindu, Ukiristo, Uislamu, Judaism na kuona mojawapo ya mambo muhimu katika maisha ni pamoja na mtu kuendeleza vizazi/koo pale anapoamua iwe hivyo ndio Rekha akasikilizwa ombi lake.

Japokuwa mume huyo amefungwa maisha kwa makosa yake lakini kwa upande mwingine mahakama imeona hali hiyo imemuathiri mke wake kihisia na haki yake ya kupata tendo la ndoa licha ya yeye kuwa na makosa lakini mke wake hana makosa yoyote ndio maana amesikilizwa.

Pia, imeelezwa kuwa kipindi cha nyuma mahakama ilimpa mwanaume huyo ruhusa ya kwenda uraiani kwa siku kadhaa halafu muda ulipoisha akarudi mwenyewe jela kuendelea kutumikia kifungo chake cha maisha hivyo alionesha nidhamu na utii wa sheria ndio maana wamempa tena siku 15 arudi uraiani kumpa ujauzito mke wake afurahie maisha yake na ya ndoa halafu mume arudi zake gerezani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live