Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyegushi vyeti vya Digrii apata kazi Benki

Kugushi Vyeti Aliyegushi vyeti vya Digrii apata kazi Benki

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtafiti wa masuala ya uhalifu wa kimitandao katika benki moja jijini Nairobi ameshtakiwa kujipatia kazi hiyo kwa kughushi cheti cha digrii katika somo la sayansi ya kompyuta kutoka chuo kikuu.

Gerald Lumuchele aliyefikishwa mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani jijini Nairobi Bw Bernard Ochoi alikana alighushi cheti hicho cha digrii kutoka Chuo Kikuu cha Moi.

Ochoi alielezwa mshtakiwa alifanya mahojiano ya kazi hiyo akiwa na watu wengine watatu kisha akawabwaga wote ndipo akaajiriwa na Benki ya Housing Finance Limited, Nairobi.

Lumuchele aliguduliwa hajahitimu kimasomo baada ya kupokea mishahara ya miezi minane akitumia digrii hiyo feki.

Kiongozi wa mashtaka Bw James Machira alieleza korti Chuo Kikuu cha Moi kiliandikia benki hiyo kusema jina la mshtakiwa halikuwa katika orodha ya wanafunzi waliohitimu katika somo la sayansi ya kompyuta.

Lumuchele alikabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi cheti cha kuhitimu na Digrii katika somo la sayansi ya kompyuta mnamo Juni 13, 2022 kutoka Chuo Kikuu cha Moi.

Mahakama ilijuzwa mshtakiwa alidai alihitimu kwa digrii hiyo mnamo Desemba 17, 2021. Mshtakiwa alimkabidhi afisa wa benki hiyo Bi Gloria Lilechi akidai amehitimu kwa digrii na yuafaa kufanya kazi hiyo.

Mshtakiwa alikana mashtaka mawili na kuchiliwa kwa dhamana ya Sh 100,000. Kesi itatajwa baada ya wiki mbili ili mshtakiwa akabidhiwe nakala za mashahidi.

Wabunge waanzisha mchakato wa kuweka NG-CDF ndani ya KatibaRipoti yaonyesha wanaume nchini Kenya wanaogopa kuoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live