Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyegomea uteuzi na wenzake wasota polisi

Aliyegomea Uteuzi Na Wenzake Wasota Polisi Aliyegomea uteuzi na wenzake wasota polisi

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japhet Maganga na wenzake tisa bado wanashikiliwa na Polisi mkoani Dodoma.

Maganga na wenzake, walikamatwa Februari 16, mwaka huu kwa kile kinachodaiwa kufanya fujo kwenye mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliofanyika jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno alisema jana kuwa bado wanawashikilia watu hao na watafikishwa mahakamani taratibu za upelelezi zitakapokamilika.

Walikamatwa juzi Alhamisi kwenye mkutano wa CWT kwa madai ya kufanya fujo baada ya Maganga kudai hana imani na mwenyekiti wake (Leah Ulaya), hivyo aliomba makamu mwenyekiti aongoze kikao hicho.

Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Taifa la CWT, Emmanuel Kihako alisema jana kuwa wamejitahidi kuwawekea dhamana watuhumiwa hao, lakini hawajafanikiwa.

Chanzo: Mwananchi