Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyefungwa miaka 7 kwa wivu wa mapenzi aachiwa huru

Hukumu Pc Data Aliyefungwa miaka 7 kwa wivu wa mapenzi aachiwa huru

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora imemfutia hatia na kifungo cha miaka saba jela, Apronia Mathew aliyedaiwa kumwagia maji ya moto Asha Musa aliyemtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mumewe.

Apronia alidaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 5,2020 na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo ambako alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Inadaiwa kwamba wakati Asha akitoa malalamiko hayo, mshitakiwa alikuwa amebandika maji ya kuoga na katika kujilinda dhidi ya mlalamikaji, alichukua maji hayo na kumwagia mwilini.

Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Athuman Matuma amesema kuwa anakubaliana na rufaa ya mshitakiwa huyo kwamba upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha mashitaka hayo.

Amesema kuwa kiwango cha majeraha aliyopata mlalamikaji hayajathibitishwa na kwamba kumwagiwa maji ya moto haitoshi kuthibitisha kwamba madhara makubwa yametokea.

Hata hivyo, upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha PF3 kuonesha ripoti ya majeraha yaliyosababishwa kwa Asha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live