Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyefungua zipu ya polisi mwanamke ashtakiwa

Felix Karani Thumbi Aliyefungua zipu ya polisi mwanamke ashtakiwa

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume aliyeshika afisa wa polisi mwanamke matiti na kupelekea mahabusu aliyekuwa amemkamata kwa kukaidi sheria za barabara kutoweka, ameshtakiwa.

Felix Karani Thumbi aliyeshtakiwa mbele ya hakimu mkazi alikanusha alimdhulumu na kumuumiza afisa huyo wa polisi mwanamke. Thumbi alikana alitenda uhalifu huo katika barabara ya Enterprise, Nairobi.

Mshtakiwa alikabiliwa na shtaka kumdhihaki afisa huyo na kupelekea mahabusu aliyekuwa amemtia nguvuni kutoroka.

Thumbi anadaiwa alimkuta mlalamishi katika mzunguko wa barabara ya Enterprise karibu na DT Dobie akiwa amemtia nguvuni dereva ambaye hakuwa na leseni.

Thumbi alianza kumchukua video afisa huyo kisha akamtaka aonyeshe nambari yake ya ajira lakini afisa huyo mwanamke akakataa.

Thumbi alimfungua zipu ya jaketi yake ndipo aone nambari ya ajira. Katika hali hiyo mshtakiwa alimshika matiti afisa huyo. Kisa hicho kiliwafanya waendeshao pikipiki kukusanyika na wapita njia pia.

Mshtakiwa aliendelea na harakati za kuchukua video lakini afisa wa polisi mwingine alimsaidia mlalamishi na kumtia nguvuni Thumbi.

Alipokana shtaka aliomba aachiliwe kwa dhamana. Mwangi amemwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh100,000. Kesi hiyo itatajwa Novemba 28, 2022 na kutengewa Aprili 13, 2023 kusikilizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live