Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyedaiwa kumuua jirani yake kwa visu ashinda kesi

Hukumu Pc Data Aliyedaiwa kumuua jirani yake kwa visu ashinda kesi

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru, dereva Boi Rajabu (65) aliyekuwa aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Rajabu anadaiwa kumuua jirani yake aitwaye, Abbas Mwinjuma kwa kumchoma kisu tumboni hadi utumbo ukatoka nje, tukio analodaiwa kulifanya Februari 8, 2019 katika eneo la Mbweni Miti mitatu, Wilaya ya Kinondoni.

Hukumu hiyo imetolewa jana, Februari 23, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

"Hakuna ushahidi wowote wa upande wa mashtaka ulionyesha kuwa Rajabu alimuua Abbas na hata mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao hapa mahakamani wamehadithiwa na Adam Matutu, ambaye upande wa mashtaka walitakiwa kumleta mahakamani ili aje atoe ushahidi, lakini kwa bahati mbaya sana hawakumleta.

"Tukio limetokea uani katika nyumba ambayo Abbas anaishi na mama yake na kutoka katika nyumba ya mtuhumiwa hadi hapo uani kwa kina Abbas ni umbali wa mita sita, kwa nini hakuna jirani yoyote wa eneo hilo aliyeenda kugonga mlago wa Boi kujua yupo au hayupo ili wamkamate?

“Kwa nini Boi alikamatwa kesho yake akiwa kwenye shughuli zake na sio usiku ule ule wa tukio?" amehoji Hakimu Mbuya.

Amesema kutoka na ushahidi wote uliotolewa hakuna ushahidi wa moja kwa moja ambao unamtia hatiani mshtakiwa.

"Mahakama imeridhika kuwa kosa linalomkabili mshtakiwa, upande wa mashtaka wameshindwa kuthibitisha, hivyo nakuachia huru," amesema Hakimu Mbuya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live