Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Thomas Magoli umedai kuwa mtuhumiwa huyo ameandika barua ya kukiri makosa na kuomba msamaha kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP), Biswalo Mganga.
Magoli anakabiliwa na makosa matatu likiwemo la kujifanya ofisa Usalama wa Taifa ili kumsaidia Rais wa zamani wa Shirikisho la Mapira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi katika kesi inayomkabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa mshtakiwa huyo alishaandika barua ya kukiri makosa kwa DPP lakini kuna baadhi ya vitu havijakamilika.
"Naiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa kuwa bado Kuna vitu havijakamilika," amedai Simon.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 21, 2019.
Katika kesi ya msingi inadaiwa katika kosa la kwanza kati ya Desemba 1, 2017 na Agosti 2019 mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijifanya mtumishi wa umma aliyeajiriwa kitengo cha Usalama wa Taifa.
Pia Soma
- Benki ya Dunia yaipatia Tanzania mkopo wa Sh1 trilioni
- Tamwa wampongeza Magufuli kukemea mimba kwa wanafunzi mkoani Rukwa
Katika kosa la tatu la utakatishaji fedha anadaiwa kutakatisha kiasi cha Sh280,000 kwa kuzitumia fedha hizo huku akijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.