Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeachiwa huru kwenye kesi ya mauaji, akamatwa kwa madai ya kuua tena

1944 Jail 660x400 Aliyeachiwa huru kwenye kesi ya mauaji, akamatwa kwa madai ya kuua tena

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamume mmoja ambaye alihukumiwa kifo kwa wizi wa kimabavu na kuachiliwa huru baada ya kukata rufaa, amekamatwa tena kwa tuhuma ya kumuua mwanamke na kuficha mwili wake ndani ya kabati.

Mwanamume huyo alihukumiwa kifo kwa wizi wa kimabavu mwaka 2016 na kuachiliwa huru baada ya kukata rufaa mwaka 2016Katika kesi ya 2016, Robert Waliaula Kinisu alikabiliwa na mashtaka ya kumuibia na kumuua mwanamitindo wa Mombasa, Janet Adhiambo Asuna.

Miaka miwili baadaye, Kinisu amekamatwa tena akituhumiwa kumuua mwanabiashara wa Mtwapa, Jacqueline Ngina Kitheka na kuficha mwili wake ndani ya kabati.

Robert Waliaula Kinisu aligonga vichwa vya habari mwaka 2016, akikabiliwa na mashtaka ya kumuibia na kumuua mwanamitindo wa Mombasa, Janet Adhiambo Asuna nyumbani kwake Kizingo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Taifa Leo, Kinisu alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo na Mahakama ya Hakimu na kisha baadaye alikata rufaa na kuachiliwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2019.

Miaka miwili baada ya kurejeshewa uhuru wake, Kinisu amekamatwa tena akituhumiwa kumuua mwanabiashara wa Mtwapa, Jacqueline Ngina Kitheka.

Kinisu anaripotiwa kumuua Kitheka na kuficha mwili wake ndani ya kabati la nguo nyumbani kwake na kutoweka na vitu vyake vya thamani ikiwemo simu.

Kitheka alikuwa mwanabiashara wa nguo Mtwapa, katika kaunti ya Kilifi na pia alikuwa akiwauzia watalii nguo za kuogelea katika ufuo wa Pirates.

Kulingana na stakabadhi zilizowasilishwa kortini, mshukiwa huyo anadaiwa kumvamia marehemu nyumbani kwake eneo la Marina, Mtwapa kabla ya kumuua na kuficha mwili wake.

Mwili wa mwanabiashara huyo ambaye alikuwa mama wa watoto wawili ulipatikana siku tatu baada ya kuuawa.

Alikuwa na njama ya kutorokea Uganda Upande wa mashtaka uliambia korti kuwa Kinisu alitenda kitendo hicho cha kinyama kati ya Mei 3 na 6, 2021.

Akipinga ombi lake la kuachiliwa kw dhamana, afisa mpelelezi wa kesi hiyo, Diba Halake aliambia mahakama kuwa mshukiwa huyo hana makazi maalum na alikuwa amepanga njama ya kutorokea Uganda wakati alikamatwa.

Jaji Anne Ong'njo alikubali ombi la upande wa mashataka na kuamua kwamba Kinisu asalie kwenye rumande.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke