Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alipukiwa na bomu lililowekwa kwenye zawadi ya harusi aliyopewa na ‘x’

BOMU EKA Alipukiwa na bomu lililowekwa kwenye zawadi ya harusi aliyopewa na ‘x’

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke na mume wamejikuta wakilipukiwa na bomu mara baada ya kufungua zawadi waliyozawadia na mpenzi wa zamani (x) wa dada yake na bibi harusi wakati wa sherehe ya harusi yao.

Jamaa huyo anayeitwa, Rajesh Patel anadaiwa kuidanganya familia hiyo kuwa angemuoa binti yao mkubwa aitwaye Jagriti kwa miaka saba lakini mwisho wa siku aliingia mitini na kumuachia kovu la maumivu ya mapenzi binti huyo ambaye tayari walikuwa wameshazaa mtoto mmoja.

Mzazi wa Salma na Jagriti aitwaye Harish Dalvi, mkazi wa mkazi wa kijiji cha Meendhabhari cha Vansada katika wilaya ya Navsari ya Gujarat nchini India amesema wakati wa harusi, Rajesh alimzawadia Salma na mumewe mdoli ambao ndani yake aliweka bomu.

Siku moja baada ya harusi kumalizika, wakati wakifungua zawadi hizo, ghafla mume wa Salma aitwaye Latesh alilipukiwa na bomu hilo na kuharibu macho yake hivyo kwa sasa hawezi tena kuona.

Akisimulia mkasa huo, Harish Dalvi amesema; “Bomu hilo lililipuka mara tu zawadi ilipofunguliwa, damu zilitapakaa pale na macho yote mawili ya mkwe wangu yameharibika, nifanye nini. sasa... naweza kutoa jicho moja kwa mkwe wangu.

"Tulianza kujiuliza ni nani aliyetoa zawadi hii. Rajesh ni mtu yule yule ambaye alimsaliti binti yangu Jagriti… Alikuwa na Jagriti kwa miaka saba na wana mtoto wa kike. Mashaka yetu yaligeuka kuwa imani kwamba mtu aliyeharibu maisha ya binti yangu mkubwa sasa anaharibu maisha ya binti yangu mdogo.

“Mkwe wangu amejeruhiwa vibaya kwenye kifundo cha mkono wa kushoto na daktari anasema macho yake pia yameharibika. Siwezi kufanya chochote zaidi kwa mkwe wangu, lakini nitampa jicho."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live