Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliemuwekea mumewe sumu kwenye chai apandishwa kizimbani

Yun Grs Aliemuwekea mumewe sumu kwenye chai apandishwa kizimbani

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari mmoja wa ngozi kutokea California nchini Marekani ambaye anatuhumiwa kwa kumuwekea sumu mumewe mara kadhaa, ameshtakiwa na jopo la Majaji.

Dr. Yue Yu anatuhumiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuweka sumu kwenye chai ya mumewe Bw. Chen kwa nia ya kumletea maumivu na mateso. Sumu hiyo ilimsababishia muhusika vidonda vya tumbo.

Mnamo mwezi Aprili mwaka jana Bw. Chen aliamua kuweka camera ndani baada ya kuanza kugundua kuwa chai aliyozoea kunywa kila siku ina ladha ya tofauti.

Baada ya kugundua kinachoendelea alichukua sampuli za chai hiyo na kupeleka Polisi ambao walizifikisha kwa FBI.

Wawili hao wamekuwa wakigombea watoto tangu mwaka jana wakati hatua za kuachana kwao zikiendelea. Hivi sasa Dr. Yu amezuiliwa kusogea karibu na mumewe na watoto wao wawili wenye umri wa miaka 9 na 8.

Ikiwa atakutwa na hatia kwa makosa yote Dr.Yul anaweza akafungwa kwa hadi miaka 8 na nusu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live