Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa akimlawiti mtoto wa binamu yake kwa kumlaghai na buku jero

Mbaroniii WA0005 Akutwa akimlawiti mtoto wa binamu yake kwa kumlaghai na buku jero

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Edgar Mkane (23) mkazi wa mtaa wa Kisiwani kata ya Kivavi mjini Makambako Njombe amekamatwa na wananchi wa mtaa huo akituhumiwa kukutwa akimbaka mtoto (binamu yake) mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba.

Akihojiwa na viongozi wa serikali ya mtaa baada ya kufikishwa ofisini, mtuhumiwa amesema alitekeleza jambo hilo baada ya tamaa wakati mtoto huyo alipofika nyumbani kwao kuangalia televisheni ambapo alimrubuni na kumuahidi kumpa kiasi cha shilingi elfu moja mia tano (Tsh/= 1500).

"Alikuja mtoto peke yake nami nikawa nimelala ndani nikaingiwa na tamaa, nikamshawishi akakubali nikamwambia nitampa 1500, kuna mwingine nilienda polisi kwa kujaribu kujaribu kufanya vile ila sikufanikiwa ni tamaa tu nami najikuta kufanya vile"amesema Edger.

Aidha, mtoto huyo mbele ya viongozi wa serikali ya mtaa amekiri kufanyiwa kitendo hicho kwa nguvu baada ya kutaa alipoenda nyumbaji kwa shangazi yake kwa lengo la kuangalia televisheni, huku Mama mzazi wa mtuhumiwa Edgar Mkane akibainisha kuwa tukio hilo ni la tatu kwa mtoto wake kutuhumiwa kulifanya ambapo amekUwa akimuonya mara kwa mara.

"Alishawahi fanya akaachiwa kupitia mikono yangu,mpaka hapa nilipo ninatetemeka yani nimemuonya mara nyingi lakini mmh! Naumia mtoto ananitia aibu," amesema mzazi.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kisiwani Rajabu Shayo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumivwa na kuiomba jamii kuacha kumaliza matukio hayo kifamilia ili kukomesha vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live