Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akutwa Amenyongwa Na Kufungwa Na Kufuli Juu Ya Mti

Video Archive
Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika kwa haraka amekutwa amening’inizwa juu ya mti mtaa wa Malingumu Mjini Mafinga huku taarifa za kifo chake zikiwa bado hazijajulikana .

Kijana huyo anayekadriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 22 ambaye kwa jina la utani anafahamika kama Babu Rungu amekutwa na umauti katika mazingira ya kutatanisha kama anavyobainisha Bi Beatrice Msigwa ambaye alikuwa mtu wa kwanza kufika kwenye tukio.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Malingumu Frida Kipangula anasema tukio hilo ni tukio la kinyama ambalo halikubaliki hivyo watekelezaji wa tukio hilo lazima watatiwa mbaroni na hakuna ataye salia salama.

Hata hivyo baada ya ya taarifa za tukio hili kulifikia jeshi la polisi, maofisa wa jeshi hilo waliwas,ili haraka eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemu kwa taratibu zaidi za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo na washtakiwa wa utekelezaji wa tukio kuanza kusakwa. Mara moja

Chanzo: globalpublishers.co.tz