Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akuhumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mkewe na mwanaye

Akuhumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Akuhumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kumuua mkewe na mwanaye

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imemuhukumu Shamswadini John (35) Mkazi wa Hanang Mkoani Manyara maarufu kama Sikukuu, kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia ambapo amemuua Mke wake aitwaye Asia John (25) na Mtoto wake Ahmedi Shamswadini (09).

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Devotha Kamzola ambapo amesema Mshtakiwa Shamswadini amemuua Mkewe kwa kumnyonga ambapo wakati akitekeleleza mauaji hayo Mtoto alikuwa akipiga kelele hivyo baada ya kumuua Mama akarudi kumuua na Mtoto, baada ya kufanya hivyo alichimba shimo kuufukia mwili wa Mkewe lakini alipotaka kuufukia mwili wa Mtoto alishindwa kwa kuhofia kuwa kumeshaanza kukucha na Watu watamuona hivyo akaamua kwenda kuutupa mwili wa Mtoto katika Bwawa ili kupoteza ushahidi.

Uchunguzi wa Daktari umeonesha ni kweli wamefariki kwa kukosa hewa baada ya kunyongwa huku Wakili wa Serikali Petro Ngassa akiiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo

Tukio hilo limetokea 31/10/2018 huko katika Kijiji cha Hideti Hanang huku chanzo cha mauaji hayo ikiwa ni ugomvi uliotokea mara baada ya Mwanaume kuongeza Mke wa pili jambo lililomchukiza Mke wa kwanza na kuamua kuhama nyumba ambapo aliamua kwenda kupanga chumba na kuanza kuishi na Mtoto wake huko ndipo Mwanaume aliposhikwa na hasira na kuhisi Mwanamke huyo kuwa na mahusiano mengine na kupelekea kutekeleza mauaji hayo.

Awali mshtakiwa alikana kuhusika na mauaji hayo lakini baadae alikiri nakwenda kuonyesha sehemu aliyofukia mwili huo wa Mkewe na baada ya kufukuliwa ulikutwa ukiwa na kanga shingoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live