Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akodisha watu wamuue Kaka yake kwa elfu 50

 Maketi Msangi Kamanda Msangi

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumuua Pankras Petro (62) mkazi wa Nyabishenge, wilayani Kyerwa, baada ya mdogo wa marehemu aitwaye Dominick Petro kuwakodisha watu watatu kwa ujira wa shilingi 50,000, ili wamuue kaka yake kutoka na mgogoro wa shamba.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Maketi Msangi, na kusema kwamba tukio la mauaji hayo lilitokea Mei 20, 2022.

"Walimjeruhi vibaya Pankras kwa kumkata na kitu cheye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, alikimbizwa hospitali ya Mission ya Isingiro na alifariki siku hiyo akipatiwa matibabu, watuhumiwa hao walikimbilia kusikojulikana, tulianza msako na kuwakamata Mei 25, 2022 baada ya kupata taarifa za siri," amesema Msangi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live