Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akatwa nyeti baada ya kushindwa kulipa Sh5,000

Akatwa nyeti baada ya kushindwa kulipa Sh5,000

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Wakati tukio la askari polisi Pc Kazimili (28) wa Shinyanga nchini Tanzania kukatwa nyeti na mke wake halijafutika masikio mwa watu, mkazi wa Nyigoti wilayani Serengeti mkoani Mara amekatwa sehemu za siri na mpenzi wake baada ya kushindwa kumlipa Sh5,000 walizoahidiana kulipana kila mshindo.

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa, Januari 10, 2020 majira ya saa 11 alfajiri katika nyumba ya kulala wageni ya Gibita iliyoko mjini Mugumu wilayani hapa.

Akizungumza kwa shida akiwa chini ya uangalizi wa waganga hospitali ya Nyerere akipata matibabu, Joseph Nyanakwi amesema alikatwa na mhudumu wa nyumba hiyo baada ya mshindo kumlipa Sh15,000 badala ya Sh20,000 walizokubaliana kulipana na kwa kila mshindo mmoja ni Sh5,000 na yeye alipiga nne na kutoa fedha pungufu.

"Kwanza tulianza kwa vinywaji kisha tukakubaliana kila (hatua) Sh5,000 lakini akaomba kwanza Sh20,000 nikalipa, tumelala kila baada ya (hatua) nilikuwa nalipa Sh5,000 mitatu nililipa huu wa nne sikulipa akanidai nikamwambia akate kwenye Sh20,000 ya kwanza akagomba.”

“Tukalala alfajiri wakati naaga niwahi kijijini kwenye kazi za uchimbaji dhahabu, kumbe alikuwa na wembe ghafla akashika sehemu yangu ya siri na kukata kuanzia chini kwenye makende ili akate kabisa nikapambana lakini akawa ameishaniumiza vibaya," amesema Nyanakwi

Amesema akapiga kelele watu wakajitokeza kumsaidia na kutoa taarifa polisi waliofika na kuwachukua wote na mhudumu huyo aliyemtaja kwa jina la Nyangi Ismael maarufu Mnyamongo ambaye polisi wamekiri kumshikilia.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Tanu Warioba amesema ataongea baada ya kumaliza kumhudumia majeruhi huyo.

Desemba 28,2019 askari polisi mwenye namba H 8980 pc Kazimili wa Shinyanga alikatwa sehemu za siri na kitu chenye ncha kali na mke wake wakati amelala kutokana na wivu wa mapenzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz