Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja mwanaume miaka 32,mkinga msanii mkazi wa sanze akiwa na silaa bandia za kivitaya,AK 47(SMG) 11,uzgan 1,Pisto 5 vest za kukingia risasi 2 zilizotengenezwa kwa plastic na mbao pamoja radio call bandia 1.
Akiongea na waandishi wa habari ofsini kwake mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani-Acp Pius Lutumo amesema katika mahojiano ya awali mtuhumiwa alikiri kuwa ametengeneza silaa hizo yeye mwenyewe na anazitumia kwa matumizi yake na mara baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Aidha, Kamanda Lutumo ametoa rai kwa kwa wananchi kuishi kwa kufuata misingi ya sheria,kama wanahitaji kutumia silaa kwa namna yoyote ile wafuate sheria na taratibu zilizowekwa za kupata vibali toka taasisi husika.