Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na polisi akiuza dawa za Serikali

52581 Pic+dawa

Tue, 16 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkazi wa Isikizya wilayani Uyui mkoani Tabora, anashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa akiwa na dawa mbalimbali za Serikali kwenye duka lake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Aprili 16,2019 amesema mkazi huyo amekamatwa akiwa na dawa za Serikali ambazo haruhusiwi kuwa nazo.

Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi na kutoa onyo kwa wananchi kutokuwa na dawa za Serikali kwenye maduka yao kwani ni kosa na watachukuliwa hatua.

Kamanda Nley amesema polisi walipata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuwa kuna mtu anauza dawa za Serikali jambo ambalo ni kosa.

Mkuu wa wilaya ya Uyui, Gift Msuya ameshukuru kwa ushirikiano wanaoutoa wananchi akisema wanafanya vizuri na kuwatia moyo waendelee kufichua maovu na waovu.

Amesisitiza kuwa ni kosa na haramu kwa mtu kuuza dawa za Serikali kwenye maduka ya madawa ya watu binafsi.

Amesema dawa za Serikali zina utaratibu wake na hazitakiwi kuuzwa kwenye maduka ya watu binafsi na anayepatikana anachukuliwa hatua za kisheria.



Chanzo: mwananchi.co.tz