Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na nyama ya pofu wanne

98734 POFU+PIC Akamatwa na nyama ya pofu wanne

Thu, 12 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kikosi cha kupambana na ujangili(KDU) Wilaya ya Kiteto kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya jamii ya wanyamapori (WMA) ya Makame iliyopo Kiteto wamemkamata mtuhumiwa wa ujangili, Masudi Mussa (33) akiwa na nyama ya pofu wanne.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Machi 11, 2020 ofisa wanyamapori  wilaya ya Kiteto, Doris Gama amesema  mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa kwa muda mrefu kutokana na kuhusika na matukio kadhaa ya ujangili.

Gama amesema alikamatwa na askari wa vikosi hivyo walioshirikiana na askari wa kupambana na ujangili wa taasisi ya Honeyguide.

“Kikosi cha doria wamemkamata na gobore moja,  pikipiki mbili, risasi sita na visu vinne,” amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz