Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na maiti yenye umri wa miaka 800

Julio Cesar .jpeg Akamatwa na maiti yenye umri wa miaka 800

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja nchini Peru amewekwa chini ya ulinzi baada ya kukutwa na maiti ya muda mrefu inayokadiriwa kuwa na umri wa miaka 800.

Picha zilizotolewa na Idara ya Utamaduni ya mji wa Puno zimeonesha mwili huo ukiwa umewekwa kwenye mfuko mwekundu ambao hutumiwa zaidi na kampuni zinazosambaza vyakula.

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Julio Cesar ameeleza kuwa alikuwa akilala na maiti hiyo chumbani kwake, kuitunza na kuichukulia kama rafiki yake wa kike akiwa ameipa jina la Juanita.

Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa mwili huo haukuwa wa mwanamke bali wa mwanaume aliyefahamika kwa jina la Juan na sio Juanita.

Tayari mwili huo umechukuliwa na kufanywa mali ya Serikali chini ya sheria za urithi wa kitaifa wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live