Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na kobe 438 wenye thamani ya milioni 71.1

Kobe Ed.jpeg Akamatwa na kobe 438 wenye thamani ya milioni 71.1

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mtuhumiwa amekamatwa na kobe hao akiwa amewahifadhi ndani ya mabegi matatu katika standi ya mabasi ya Dutwa wilayani Bariadi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao, amesema  mtuhumiwa huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa mbili usiku akiwa katika standi hiyo akisubiri usafiri ili kuendelea na safari yake ambapo hakutaka kueleza wapi alikuwa anawapeleka .

Kamanda Abwao amesema kobe hao wote wamewakabidhi kwa Maafisa Maliasili kwa ajili ya hifadhi na kwamba mtuhumiwa yuko mahabusu na atafikishwa Mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

Aidha, kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na umiliki wa nyara za serikali kinyume na sheria kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai, na pia amewaomba Wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu katika maeneo ya makazi yao ili kuendelea kuufanya Mkoa kuwa mahali salama.

Chanzo: ippmedia.com