Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na kete 2,401 dawa za kulevya Z'bar

DAWA ZA KULEVYA 2 Akamatwa na kete 2,401 dawa za kulevya Z'bar

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Nungwi kisiwani Zanzibar, Athumani Akida Juma (32) amekamatwa na pakiti 20 zenye kete 2,401 zinazodaiwa ni dawa za kulevya aina ya heroin.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Buruhani Zuberi Nassoro wakati akizumgumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Septemba 22, 2022 mjini Unguja.

Amesema kijana huyo amekamatwa katika operesheni na doria za ukamataji wahalifu wanojihusisha kuuza na kusambaza dawa ya kulevya nchini.

“Pia katika operesheni hiyo tumekamata mzigo kisiwani Pemba uliotelekezwa ukiwa na kete 4,000 za bangi huku upelelezi ukiendelea kwa kutafuta mwenye mzigo huo,” amesema

Kanali Nassoro amesema kuwa wataendelea kushirikiana na mamlaka zote zinazohusika kudhibiti vitendo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live