Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa na Polisi kwa kuua wakwe zake

Issa Njombe Ed.webp Akamatwa na Polisi kwa kuua wakwe zake

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

???????JESHI la Polisi mkoani Njombe linamshikilia Patrick Ngailo, mkazi wa Mlangali wilayani Ludewa mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya wakwe zake akiwatuhumu kuwa ni washirikina wanaomsababishia maradhi ya mara kwa mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema kijana huyo ametenda kosa hilo Juni 8, mwaka huu majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Mlangali na baada ya kutenda tukio hilo mtuhumiwa alikimbia.

“Baada ya kufanya mauaji haya mtuhumiwa alikimbia, lakini wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamemkamata” amesema Kamanda Issa.

Hata hivyo, Kamanda Issa amesema baada ya uchunguzi imebainika kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuoa mtoto wa marehemu hao alianza kupatwa na maradhi mara kwa mara hivyo akaamua kuchukua uamuzi wa kwenda kwa mganga ndipo akaelezwa kuwa maradhi hayo yanatokana na mke wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live