JESHI la polisi Mkoani Katavi, linamshikilia Jilangu Seni (33) mkazi wa kijiji cha Misisi, kwa tuhuma za kukutwa na kipande kimoja cha jino la tembo ambacho alikuwa amekificha juu ya chumba anachoishi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 6, 2022, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi, Ali Hamad, amesema tukio hilo lilitokea Januari 2 mwaka huu katika kijiji cha Misisi wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Kamanda Hamad amesema mtuhumiwa alikuwa amelihifadhi jino hilo kwenye mfuko wa salfeti na kulificha juu ya dari ya nyumba anayoishi.
Amesema thamani ya jino hilo bado haijatambulika na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa baada ya upelelezi kukamilika jalada litafikishwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria.