Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa kwa wizi wa mtoto Mwanza

Kichanga Pic Akamatwa kwa wizi wa mtoto Mwanza

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Prisca Clement kwa tuhuma za kuiba mtoto wa mwaka mmoja na miezi tisa aliemuiba Zanzibar alikokuwa akifanya kazi za ndani.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbrod Mtafungwa amesema, mwanamke huyo alikamatwa na Polisi katika kijiji cha Ntundu Kata ya Busanji Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya mwanamke huyo miaka 25, kutoweka na mtoto huyo.

Mtoto huyo aliibiwa Julai 10 mwaka huu visiwani Zanzibar, baada ya mzazi wa mtoto huyo kumuachia mtoto amwangalie ndipo mtuhumiwa alipata nafasi ya kukimbia na mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live