Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa kwa wakala na fedha bandia

FEDHA WEB Akamatwa kwa wakala na fedha bandia

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara, linamshikilia, Husseni Geni (32), mkazi wa Kijiji cha Kijungu wilayani humo kwa tuhuma za kukutwa na fedha bandia kiasi cha Tsh 240,000 ambazo alitaka kutuma kwa wakala wa fedha.

Tukio hilo limetokea Novemba 4, 2022, kwa wakala wa fedha Ndaleta usiku wa saa 2:00 kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alitaka kuweka fedha hizo kwenye akaunti yake ya simu.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Ndaleta Ijumaa Bakari, akizungumzia tukio hilo alisema mtuhumiwa alifikishwa ofisini kwake na wakala huyo wa fedha jina limehifadhiwa wakiwa na fedha hizo bandia na baada ya kuulizwa alisema kuwa ni zake naye alipewa.

Alisema baada ya kukiri aliagiza mtuhumiwa afikishwe kituo cha Polisi Kibaya kwa hatua zaidi za kisheria

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amethibitisha tukio hilo na kuwataka wananchi kuwa makini kutambua fedha bandia na kutoa taarifa Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live