Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa kwa tuhuma za kumbaka mjamzito

MIMBA WEB 111 Akamatwa kwa tuhuma za kumbaka mjamzito

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamshikilia Mohamed Mwanjali mkazi wa Mtaa wa Kitanzini kwa tuhuma za kumbaka Mama mjamzito na kumsababishia umauti.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni Kata ya Kitanzini Yassin Kisogole amesema Mwanamke huyo alitendewa ukatili huo usiku wa kuamkia September 25,2022 wakati Mumewe akiwa Mtaa wa jirani alipokwenda kushuhudia pambano la ndondi la Mandonga vs Abeid kisha la Twaha Kiduku vs Abdo kupitia TV.

Shemeji wa Marehemu aitwaye Prosper Kileo amesema Mume huyo aliporudi nyumbani baada kuangalia pambano la ngumi alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi wakati akiingia ndani alimuona Mtuhumiwa akitoka katika moja ya chumba na kukimbia ndipo alipojaribu kumkimbiza bila mafanikio.

Alipoingia ndani alimkuta Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimmsimulia kwa kumwambia “Baba alikuja Mtu hapa akamziba Mama mdomo akamuangusha chini"

Baada ya taarifa hizo Mume huyo wa Marehemu alienda kutoa taarifa Polisi, taarifa za awali zinadai Mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na Marehemu kutokana na kumripoti katika mamlaka za usalama kwa tabia za wizi, Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi nyumbani kwake ambako amekutwa na baadhi ya vitu vya Marehemu ikiwamo simu ya mkononi na nguo (suti) ambazo alizichukua mara baada ya kutekeleza tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live